• HABARI MPYA

  Wednesday, September 07, 2022

  TWIGA STARS YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA COSAFA


  TANZANIA imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya COSAFA kwa Wanawake baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Malawi kwenye mchezo wa Kundi C leo Uwanja wa Isaac Wolfson mjini Port Elizabeth nchini Afrika Kusini.
  Mabao ya Twiga Stars inayofundishwa na kocha Bakari Shime yamefungwa na Deonisia Minja dakika ya 19, Diana Lucas 
  dakika ya 45 na Opa Clement dakika ya 58, wakati la Malawi limefungwa na Asimenye Simwaka dakika ya 65.
  Twiga Stars ambao ndio mabingwa watetezi wanafikisha pointi saba baada ya mechi tatu, wakishinda mbili, nyingine dhidi ya Comoro 3-0 na sare ya 0-0 dhidi ya Botswana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  Anonymous said... September 8, 2022 at 4:41 AM

  Sasa hii ndo Timu sioTaifa stars Wanaotuangusha kila kukicha

  Item Reviewed: TWIGA STARS YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top