• HABARI MPYA

  Saturday, September 10, 2022

  MAYELE APIGA HAT TRICK YANGA YAICHAPA ZALAN 4-0


  TIMU ya Yanga SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini ambayo ilikuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Shujaa wa Yanga SC alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fiston Kalala Mayele aliyefunga mabao matatu dakika za 47, 84 na 87 na kutoa pasi ya bao lingine lililofungwa na kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' dakika ya 54.
  Timu hizo zitarudiana Septemba 17 hapo hapo Benjamin Mkapa na mshindi wa jumla atakutana na shindi kati ya St. George ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA HAT TRICK YANGA YAICHAPA ZALAN 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top