• HABARI MPYA

  Monday, September 19, 2022

  AZAM FC WAENDA KUCHEZA NA TP MAZEMBE NDOLA


  KLABU ya Azam FC inatarajiwa kwenda Jijini Ndola nchini Zambia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya TP  Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Septemba 23, mwaka huu.
  Mchezo huo unakuja kufuatia mwaliko maalum walioupata kutoka kwa miamba hiyo ya Afrika, ambao wako kambini jijini humo wakijiandaa na msimu mpya.
  Kikosi cha Azam FC, kinatarajia kusafiri kuelekea nchini humo, Alhamisi kwa ajili ya kwenda kucheza mchezo huo, ambao ni kipimo tosha kwao katika kujiandaa na mechi za Kombe la Shirikisho Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAENDA KUCHEZA NA TP MAZEMBE NDOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top