WENYEJI, Arsenal jana wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Aston Villa 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Gabriel Jesus dakika ya 40 na Gabriel Martinelli dakika ya 77 akimtungua kipa wa zamani wa The Gunners, Emiliano Martinez na bao pekee la Aston Villa limefungwa ma Douglas Luiz dakika ya 74.
Arsenal baada inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City.
0 comments:
Post a Comment