• HABARI MPYA

  Tuesday, January 04, 2022

  NAMUNGO FC YAENDELEZA VIPIGO KOMBE LA MAPINDUZI


  TIMU ya Namungo imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuwachapa wenyeji, Yosso Boys 2-0 katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 53 na Relliant Lusajo dakika ya 90 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita kufuatia kuilaza Meli 4 City katika mchezo wa kwanza Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAENDELEZA VIPIGO KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top