• HABARI MPYA

  Thursday, January 20, 2022

  MISRI YAICHAPA SUDAN 1-0 NA KUSONGA MBELE AFCON


  TIMU ya taifa ya Misri imefanikiwa kufuzu Hatua ya mtoano Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan, bao pekee la beki wa kati, Mohamed Abdelmoneim dakika ya 38 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D usiku wa Jumatano Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, Cameroon.
  Mechi nyingine ya Kundi D, Nigeria imeendeleza ubabe kwa kuichapa Guinea-Bissau 2-0, mabao ya Umar Sadiq Mesbah dakika ya 56 na William Paul Troost-Ekong dakika ya 75.
  Nigeria inamaliza kileleni na pointi zake tisa, ikifuatiwa na Misri pointi sita na zote zinasonga mbele, wakati Sudan na Guinea-Bissau zilizomaliza na pointi moja kila moja zinarejea nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISRI YAICHAPA SUDAN 1-0 NA KUSONGA MBELE AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top