• HABARI MPYA

  Sunday, January 16, 2022

  DODOMA JIJI YATOA SARE NA GEITA 1-1 JAMHURI

  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa jana Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Geita walitangulia kwa bao la Daniel Lyanga dakika ya 75, kabla ya Waziri Junior kuisawazishia Dodoma Jiji FC dakika ya 90.
  Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji wanafikisha pointi 17 katika nafasi ya tano na Geita Gold inatimiza pointi 13 katika nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YATOA SARE NA GEITA 1-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top