• HABARI MPYA

  Sunday, January 16, 2022

  CHICO USHINDI MCHEZAJI MPYA YANGA SC


  KLABU ya Yanga imemtambulisha winga Mkongo, Chico Ushindi Wa Kubanza kuwa klabu ya TP Mazembe ya kwao, Kinshasa kuwa mchezaji wake mpya wa sita dirisha hili dogo ambalo limefungwa jana Saa 6:00 usiku.
  Ushindi anakuwa mgeni wa kwanza dirisha hili dogo baada ya awali kusajiliwa wageni watano, ambao ni kipa Abdultwalib Mshery, beki beki Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ kutoka KMKM ya Zanzibar, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC, winga Dennis Nkane kutoka Biashara United na mshambuliaji Crispin Ngushi kutoka Mbeya Kwanza.


  Pamoja na Ushindi mwenye umri wa miaka 26, Yanga pia imemtambulisha Mbrazil, Milton Nienov kuwa kocha wake mpya wa makipa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHICO USHINDI MCHEZAJI MPYA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top