• HABARI MPYA

  Friday, January 28, 2022

  AZAM, NAMUNGO NA PAMBA ZASONGA MBELE ASFC


  BAO la Nahodha, beki mkongwe Aggrey Morris dakika ya 30 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Transit Camp katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inakwenda Hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ambako itamenyana na timu ya Daraja la Kwanza, Bagamoyo Friends iliyoitoa Catamine jana.
  Mechi nyingine za leo za 
  Azam Sports Federation Cup, Namungo FC imeitoa Lindi United kwa kuichapa 2-0 Uwanja wa Ilulu mjini Lindi na Pamba FC imeitoa Stand United kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mabao yote ya Namungo leo yamefungwa kwa penalti na Shiza Kichuya na Ibrahim Mkoko, wakati ya Pamba yamefungwa na Willy Magai na Moses Msukanywele .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM, NAMUNGO NA PAMBA ZASONGA MBELE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top