• HABARI MPYA

  Monday, January 17, 2022

  REAL MADRID WATWAA SUPER CUP YA 12 HISPANIA


  TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kutwaa taji la Super Cup Hispania baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao Jumapili Uwanja wa King Fahd International Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
  Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Luka Modric dakika ya 38 na la penalti la Karim Benzema dakika ya 52, ingawa wakamaliza pungufu kufuatia Eder Militao kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 87.
  Hilo linakuwa taji la 11 ya Spanish Super Cup kwa Real Madrid na kabla ya hapo mara ya mwisho walitwaa mwaka 2020, kabla ya kufungwa na Athletic Bilbao kwenye Nusu Fainali ya michuano hiyo msimu uliopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID WATWAA SUPER CUP YA 12 HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top