• HABARI MPYA

  Thursday, January 20, 2022

  MAN UNITED YAWACHAPA BRENTFORD 3-1 MIDDLESEX


  TIMU ya Manchester United imewazima wenyeji, Brentford kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Brentford Community mjini Brentford, Middlesex.
  Mabao ya Man United yamefungwa na Anthony Elanga dakika ya 55, Mason Greenwood dakika ya 62 na Marcus Rashford dakika ya 77 akimaliza ukame wa mabao uliomuandama kwa muda mrefu, wakati bao pekee la Brentford limefungwa na Ivan Toney dakika ya 85.
  Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 35 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya saba ikizidiwa wastani wa mabao tu na Arsenal ambayo pia mechi moja mkononi, wakati Brentford inabaki na pointi zake 23 za mechi 22 katika nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAWACHAPA BRENTFORD 3-1 MIDDLESEX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top