• HABARI MPYA

  Monday, January 17, 2022

  LIVERPOOL YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA ENGLAND


  WENYEJI, Liverpool wamefufua matumaini ya ubingwa baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumapili Uwanja wa at Anfield.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Fabinho dakika ya 44, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 69 na Takumi Minamino dakika ya  77 na kwa ushindi huo kikosi cha Jurgen Klopp kinafikisha pointi 45 katika mchezo wa 21, kikizidiwa pointi 11 na mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
  Brentford yenyewe inabaki na pointi zake 23 za mechi 21 katika nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top