• HABARI MPYA

    Monday, January 17, 2022

    ALGERIA WAWEKA KOMBE REHANI AFCON, IVORY COAST...


    MABINGWA watetezi, Algeria wamejiweka njia panda baada ya kuchapwa 1-0 na Equatorial Guinea bao la Esteban Obiang dakika ya 70 katika mchezo wa Kundi E usiku wa Jumapili Uwanja wa Douala nchini Cameroon.
    Mechi nyingine ya kundi hilo, Ivory Coast ililazimishwa sare ya 2-3 na Sierra Leone hapo hapo Douala.
    Mabao ya Ivory Coast yalifungwa na Sébastien Haller dakika ya 25 na Nicolas Pépé dakika ya 69, wakati ya Sierra Leone yalifungwa na Musa Noah Kamara dakika ya 55 na Alhaji Kamara dakika ya 90.
    Sasa Ivory Coast inaongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na Equatorial Guinea pointi tatu, Sierra Leone pointi mbili, wakati Algeria yenye pointi moja inashika mkia.
    Mechi nyingine za Jumapili AFCON, Gambia ilitoa sare ya 1-1 na Mali, wakati Tunisia iliitandika Mauritania 4-0 zote za Kundi F Uwanja wa Limbe.
    Mali ilitangulia kwa bao la Ibrahima Koné dakika ya kabla ya Musa Barrow kuisawazishia Gambia dakika ya 90, wote wakifunga kwa penalti wakati mabao ya Tunisia yalifungwa na Hamza Mathlouthi dakika ya nne, Wahbi Khazri dakika ya nane na 64 na Seifeddine Jaziri dakika ya 66.
    Sasa Gambia una Mali zinafikisha pointi nne, zikifuatiwa na Tunisia pointi tatu na Mauritania ambayo haina pointi na imeshatolewa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALGERIA WAWEKA KOMBE REHANI AFCON, IVORY COAST... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top