• HABARI MPYA

  Tuesday, January 18, 2022

  REFA MTANZANIA KAZINI AFCON GABON NA MOROCCO


  MWAMUZI Mtanzania, Frank Kombe leo atapeperusha kibendera chake kwenye mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baina ya Gabon na Morocco kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, Cameroon.
  Katika mchezo huo, Gabon watawakosa nyota wao wawili, Pierre-Emerick Aubameyang na Mario Lemina ambao wamerejeshwa kwenye klabu zao baada ya kupatwa na matatizo ya moyo ‘heart lesions’, au vidonda vya moyo wakiwa kwenye AFCON.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Gabon imesema kwamba, Aubameyang, mshambuliaji wa Arsenal ya England na Lemina, kiungo wa Nice ya Ufaransa, watakwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi na klabu zao.

  MECHI ZOTE ZA LEO AFCON - LIVE AZAM TV

   
  ZimbabweSaa 1:00Guinea        ZBC 2
   
  MalawiSaa 1:00Senegal       UTV
   
  GabonSaa 4:00Morocco       UTV
   
  GhanaSaa 4:00Comoro        ZBC 2

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA MTANZANIA KAZINI AFCON GABON NA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top