• HABARI MPYA

  Monday, January 31, 2022

  MAN UNITED YAMSIMAMISHA MASON GREENWOOD


  KLABU ya Manchester United imetangaza kumsimamisha kwa muda mshambuliaji wake, Mason Greenwood ambaye anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga mpenzi wake, Harriet Robson.
  Harriet aliposti katika ukurasa wake wa Instagram clip ya sauti na video za mwili wake zinazoonyesha namna alivyopigwa na mchezaji huyo wa Man U na Polisi imethibitisha kumshikilia Greenwoon.
  “Mason Greenwood hatarejea kwenye mazoezi au kucheza mechi hadi ikapotangazwa. Tunafahamu picha na tuhuma zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii. Hatutatoa maoni yoyote zaidi hadi ukweli utakapothibitishwa. Manchester United haikubaliani na vurugu za aina yoyote,” " Imesema taarifa ya Man U.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAMSIMAMISHA MASON GREENWOOD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top