• HABARI MPYA

  Tuesday, January 11, 2022

  NIGERIA YAICHAPA MISRI 1-0, ALGERIA YASHIKWA AFCON


  TIMU ya taifa ya Nigeria imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Misri leo, bao pekee la mshambuliaji wa Leicester City, Kelechi Iheanacho dakika ya 30 katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua.
  Nao mabingwa watetezi, Algeria wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Sierra Leone katika mchezo wa Kundi E Uwanja wa Japoma Jijini Douala.
  Mechi nyingine ya Kundi D,  Sudan imetoka sare ya bila kufungana na Guinea-Bissau Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIGERIA YAICHAPA MISRI 1-0, ALGERIA YASHIKWA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top