• HABARI MPYA

  Wednesday, January 19, 2022

  MUKOKO AFUNGA PENALTI MBILI, YANGA YASHINDA 2-0 ARUSHA


  VINARA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbuni FC ya Monduli katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Mabao yote ya Yanga yamefungwa na kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mukoko Tonombe aliyekuwa anacheza kama sentahafu leo.
  Tonombe amefunga mabao yote hayo kwa penalti kipindi cha pili, la kwanza baada ya beki wa Mbuni kuunawa mpira kwenye boksi dakika ya 56 na la pili baada ya Mkongo mwenzake, Chico Ushindi kuangushwa kwenye boksi dakika ya 82.


  Ushindi amecheza mechi ya kwanza Yanga leo baada ya kusajiliwa mwishoni mwa wiki kutoka TP Mazembe ya kwao, Kinshasa.
  Yanga imeutumia mchezo huu kama sehemu ya maandalizi ya mechi yake ijayo ya Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania Jumapili Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUKOKO AFUNGA PENALTI MBILI, YANGA YASHINDA 2-0 ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top