• HABARI MPYA

  Friday, January 14, 2022

  RUVU SHOOTING YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA 1-1 MABATINI


  WENYEJI, Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Ruvu walitangulia kwa bao la Abalkassim Suleiman Ali dakika ya 78, kabla ya Ibrahim Ame Mohamed kuisawazishia Mtibwa dakika ya 82.
  Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi 11 baada ya mechi 12, Mtibwa ikiwa nafasi ya 11 kutokana na kuizidi Ruvu wastani wa mabao, ambayo inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA 1-1 MABATINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top