• HABARI MPYA

  Friday, January 21, 2022

  JAMAA WA IGUNGA ASHINDA JACKPOT BONUS SH. MILIONI 21.7


  MKAZI wa Masanga, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora Elibariki Edson Magaa,(33) ameibuka mshindi wa Jackpot Bonus ya Sportpesa kwa wikiendi iliyoisha baada ya kupatia kwa usahihi ubashiri wake wa mechi 12 kati ya mechi 13.
  Elibariki Magaa ambaye ni msanii wa fani ya kuchora na usanifu aliweka mkeka wake wa Jackpot usiku wa kuamkia Tarehe 15 mwezi huu na kufanikiwa kushinda kitita cha shilingi 21,731,100 na kuwa mshindi pekee wa Jackpot Bonus kwa timu 12, kwa wiki iliyoisha.
  Akizungumza baada ya utambulisho na makabidhiano ya mfano wa hundi ya malipo yake, Magaa anasema yeye alianza kucheza na Sportpesa miaka mitatu iliyopita. Anasema kuwa pamoja ya kwamba yeye pia ni mchezaji wa michezo ya kubahatisha na kampuni nyingine, alivutiwa sana na Odds pamoja na kiwango kukubwa cha Bonus ambazo hakuna kampuni nyingine inazitoa’’.
  Anaendelea kwa kusema ‘ kuwa yeye huwa anacheza zaidi Jackpot na tangu ameanza kucheza hii ndio mara yake ya kwanza ameshinda kiwango kikubwa cha pesa. ‘’Ni maajabu kweli kweli, kwani uwezo wangu wa kushinda mechi ulikuwa ni wastani wa mechi nane hadi tisa, haya ni mafanikio makubwa sana kwangu kwa kuweza kufikisha mechi 12’’.
  Nakumbuka siku ya Ijumaa iliyopita, ilipofika mida ya alasiri, nilifungua app ya Sportpesa na kuchagua mechi na kuziacha bila kuweka ubashiri. Lakini ilipofika usiku wa manane niliona ni muda muafaka wa kuweka mkeka wangu kabla sijalala. Kilichofuatia ndio huu ushindi wa Jackpot Bonus ya mechi 12.
  Bwana Elibariki alichukua fursa hiyo kuwaasa watanzania wenzake kuwa ili uweze kushinda ni lazima uwekeze muda na pesa kiasi ili uweze kufuatilia timu kwenye kila hatua pamoja na kufanya mchanganuo wa kimahesabu kwenye odds. ‘’ Mimi huwa sitegemei bahati kwa asilimia mia moja. Huwa napoteza muda wangu sana usiku wa manane usiku ili kuwa na uhakika na ninachofanya.
  Naye Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Sportpesa Sabrina Msuya amesema kwa wiki hiii Jackpot imesimamia Tshs 861,636,800 hivyo amewaasa watanzania kuendelea kucheza zaidi Jackpot ili na wao wapate fursa ya kushinda kama  ambavyo Elibariki na wengine waliokwisha shinda.
  Kupata taarifa zaidi kutusu Washindi wa Jackpot bonyeza hapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JAMAA WA IGUNGA ASHINDA JACKPOT BONUS SH. MILIONI 21.7 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top