• HABARI MPYA

  Saturday, January 22, 2022

  SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA MTIBWA MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wameambulia sare kwa mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mangunu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mtibwa Sugar inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya 13, wakati Simba SC inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 12, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi saba na watani wa jadi, Simba baada ya timu zote kucheza mechi 12.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Azam FC imewatandika wenyeji, Tanzania Prisons 4-0, mabao ya Tepsi Evance dakika ya 27, Ismail Aziz Kader dakika ya 68, Ibrahim Ajibu dakika ya 70 na Justin Zullu dakika ya 82 Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Nayo Biashara United imelazimishwa sare ya bila kufungana na Geita Gold Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Azam FC inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya nne, ikizidiwa pointi moja na Mbeya City baada ya timu zote kucheza mechi 13, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 11 za mechi 13 na sasa inahamia mkiani.
  Biashara United inafikisha pointi 11 katika mechi ya 13 nafasi ya 14 na Geita Gold sasa ina pointi 14 za mechi 13 pia nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA MTIBWA MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top