• HABARI MPYA

  Sunday, January 23, 2022

  MAN CITY YAPUNGUZWA KASI ST. MARY'S


  MABINGWA watetezi, Manchester City usiku wa jana wamelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. Mary's.
  Southampton walitangulia kwa bao la Kyle Walker-Peters dakika ya saba, kabla ya Aymeric Laporte kuisawazishia Man City dakika ya 65.
  Sare hiyo inaifanya Man City ifikishe pointi 57 katika mchezo wa 23 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 12 zaidi ya Liverpool wanaofuatia ambao pia wana mechi mbili mkononi, wakati Southampton wanafikisha pointi 25 katika mechi ya 22 na kusogea nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAPUNGUZWA KASI ST. MARY'S Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top