• HABARI MPYA

    Wednesday, January 19, 2022

    COMORO YAICHAPA GHANA 3-2 NA KUITUPA NJE AFCON


    TIMU ya taifa ya Comoro imeitupa Ghana nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuichapa mabao 3-2 katika mchezo wa mwisho wa Kundi C usiku wa Jumanne Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua, Cameroon.
    Mabao ya Comoro yalifungwa na El Fardou Mohamed Ben Nabouhane dakika ya nne na Ahmed Mogni mawili, dakika ya 61 na 85, wakati ya Ghana iliyomaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Andre Ayew kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 25, yalifungwa na Richmond Boakye dakika ya 64 na Alexander Djiku dakika ya 77.
    Mechi nyingine ya Kundi C, Gabon imetoa sare ya  2-2 na Morocco Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé.
    Mabao ya Gabon yamefungwa na Jim Émilien Ngowet Allevinah dakika ya 21 na Nayef Aguerd aliyejifunga dakika ya 81, wakati ya Morocco yalifungwa na Sofiane Boufal dakika ya 74 kwa penalti na Achraf Hakimi dakika ya 84.
    Morocco inamaliza kileleni kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Gabon pointi tano na zote zinasonga mbele, wakati Comoro iliyomaliza na pointi tatu nafasi ya tatu na Ghana pointi moja mkiani zote zinarejea nyumbani.
    Mapema jioni mechi za Kundi B; Zimbabwe iliichapa Guinea 2-1 Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé na Malawi ilitoa sare ya bila mabao na Senegal Uwanja wa 
    Mabao ya Zimbabwe yalifungwa na Knowledge Musona dakika ya 26 na Kudakwashe Mahachi dakika ya 43, wakati la Guinea lilifungwa na Naby Keïta dakika ya 49.
    Kwa matokeo hayo, Senegal inamaliza kileleni kwa pointi zake tano, ikifuatiwa na Guinea pointi nne na zote zinasonga mbele, wakati Malawi iliyomaliza na pointi nne pia na Zimbabwe pointi tatu zinapanda ndege kurejea nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COMORO YAICHAPA GHANA 3-2 NA KUITUPA NJE AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top