• HABARI MPYA

  Sunday, January 09, 2022

  CAMEROON YAICHAPA BURKINA FASO 2-1 UFUNGUZI AFCON


  WENYEJI, Cameroon wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaounde.
  Mabao yote ya Cameroon yamefungwa na mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Vincent Aboubakar kwa penalti dakika ya 40 na 45 baada ya Burkina Faso kutangulia kwa bao Gustavo Sangare  dakika ya 25.
   
  Mechi nyingine ya Kundi A leo, bao pekee la Júlio Tavares dakika ya 45 na ushei liliwapa Cape Verde ushindi wa 1-0 dhidi ya Ethiopia hapo hapo Uwanja wa Paul Biya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YAICHAPA BURKINA FASO 2-1 UFUNGUZI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top