• HABARI MPYA

  Saturday, January 29, 2022

  MAYELE AIPELEKA YANGA 16 BORA KOMBE LA TFF


  VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza jioni ya leo.
  Bao pekee la Yanga leo limefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Mkongo Fiston Kalala Mayele dakika ya 54 kwa kichwa akimalizia krosi maridadi ya kiungo  mzawa, Farid Mussa Malik kutoka kulia.
  Matokeo ya mechi nyingine ya 32 Bora ASFC leo, Ruvu Shooting imeitoa KMC kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji l Dar es Salaam.
  KMC ilianza vizuri kwa kutangulia na bao la Iddi Kipagwile, kabla ya Abrahaman Mussa kuisawazishia Ruvu Shooting na kwenye mikwaju ya penalti kipa Benedict Tinocco alipngua shuti la Kenny Ally.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE AIPELEKA YANGA 16 BORA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top