• HABARI MPYA

  Monday, January 10, 2022

  SADIO MANE AING’ARISHA SENEGAL AFCON


  TIMU ya taifa ya Senegal imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa y Afrika  baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zimbabwe bao pekee la nyota wa Liverpool, Sadio Mane dakika ya mwisho katika mchezo wa Kundi B leo Uwanja wa Bafoussam mjini Bafoussam, Cameroon.
  Mane alifunga kwa penalti dakika ya saba ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 baada ya beki Kelvin Madzongwe kuunawa mpira.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, Guinea pia imeshinda 1-0 dhidi ya Malawi bao pekee la beki wa Toulouse ya Ufaransa, Issiaga Sylla dakika ya 36 hapo hapo Bafoussam.
  Nayo Morocco imeichapa Ghana 1-0 pia, bao pekee la kiungo wa Angers ya Ufaransa, Sofiane Boufal dakika ya 83 katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde.
  Mechi nyingine ya Kundi C, bao la mshambulaji wa Al Arabi ya Qatar, Aaron Salem Boupendza Pozzi dakika ya 16 limeipa Gabon ushindi wa 1-0 dhidi ya Comoro hapo hapo Ahmadou Ahidjo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SADIO MANE AING’ARISHA SENEGAL AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top