• HABARI MPYA

  Thursday, January 27, 2022

  SIMBA SC WAREJEA KUPOZA MACHUNGU KWA DAR CITY


  MSHAMBULIAJI Mkongo wa Simba SC, Chris Kope Mutshimba Mugalu aliteremka kwenye ndege baada ya ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kutoka Bukoba ambako jana walifungwa 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba.
  Simba SC itateremka tena dimbani Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salam kumenyana na Dar City katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Ikumbukwe Simba haijapata ushindi katika mechi tatu zilizopita kufuatia kufungwa 1-0 mara mbili, nyingine na Mbeya City na sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar, zote ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAREJEA KUPOZA MACHUNGU KWA DAR CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top