• HABARI MPYA

  Sunday, January 23, 2022

  MISRI NA SENEGAL, NIGERIA NA GHANA KUFUZU QATAR

  MAGWIJI wa soka barani, El Hadji Diouf wa Senegal na Emmanuel Adebayor wa Togo jana waliongoza droo ya Raundi ya mwisho ya mchujo wa Afrika kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia baadaye mwaka nchini Qatar.
  Katika droo hiyo, Misri itamenyana na Senegal, Cameroon na Algeria, Ghana na Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Morocco na Mali dhidi ya Tunisia.
  Washindi watano wa mechi hizo zitakazochezwa Machi mwaka huu ndio watakaoiwakilisha Afrika katika Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.
  Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Machi 24 na 26 na marudiano kati ya Machi 27 na 29 na Misri, Cameroon, Ghana, DRC na Mali zote zitaanzia nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISRI NA SENEGAL, NIGERIA NA GHANA KUFUZU QATAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top