• HABARI MPYA

  Sunday, January 16, 2022

  NIGERIA YASONGA MBELE, MISRI YAZINDUKA AFCON


  TIMUya taifa ya Nigeria imefuzu hatua ya mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Sudan katika mchezo wa Kundi D usiku wa jana Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua, Cameroon.
  Mabao ya Super Eagles yamefungwa na Samuel Chukwueze dakika ya tatu, Taiwo Awoniyi dakika ya 45 na Moses Simon dakika ya 46, wakati bao pekee la Sudan limefungwa na Walieldin Khedr kwa penalti dakika ya 70.
  Mechi nyingine ya kundi hilo, bao pekee la Mohamed Salah dakika ya 69 liliipa Misri ushindi wa 1-0 dhidi ya Guinea-Bissau hapo hapo Roumdé Adjia na kuweka hai matumaini ya kusonga mbele kuelekea mechi ya mwisho dhidi ya Sudan.
  Sasa Nigeria ina pointi sita, ikifuatiwa na Misri pointi tatu, wakati Guinea-Bissau na Sudan kila moja ina pointi moja kuelekea mechi zao za mwisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIGERIA YASONGA MBELE, MISRI YAZINDUKA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top