• HABARI MPYA

  Monday, January 17, 2022

  TASWA YAANZA KUANDIKISHA UPYA WANACHAMA


  CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kimeanza mchakato wa kuandikisha wanachama wapya na kuhuisha wanachama wa zamani, ili kuelekea kufanya uchaguzi Mkuu wa kupata viongozi wapya watakaokiongoza chama kwa miaka minne ijayo.
  Taarifa ya Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto leo imesema kwamba wamepokea maelekezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa(BMT), kuandaa rejesta ya wanachama na kuiwasilisha BMT hadi kufikia Februari 15 mwaka huu, kwa hatua nyingine za kupanga Uchaguzi Mkuu.
  Pinto amesema TASWA inawaomba wanachama wake wote kuhuisha uanachama wao kwa kulipia ada kuanzia leo hadi Februari 15, mwaka huu pia inawahamasisha waandishi wa habari za michezo ambao si wanachama, lakini wanataka kuwa wanachama wajitokeze kuomba uanachama kwa muda huo uliowekwa.
  "Ili kurahisisha jambo hilo la kuandaa rejesta ya wanachama liwe na ufanisi zaidi, kutakuwa na waratibu wawili, ambao ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba ya TASWA, Gift Macha na Mhazini Msaidizi wa TASWA, Zena Chande watakaotekeleza jukumu hilo chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu wa TASWA, (Amir Mhando),"amesema Pinto.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TASWA YAANZA KUANDIKISHA UPYA WANACHAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top