• HABARI MPYA

  Monday, January 10, 2022

  NI SIMBA NA AZAM FAINALI MAPINDUZI ALHAMISI


  MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Namungo FC usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 15 na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 50 na sasa watakutana na Azam FC waliowatoa mabingwa watetezi, Yanga SC kwa penalti 9-8 kufuatia sare ya 0-0 leo hapo hapo Amaan. Fainali itachezwa Alhamisi Saa 2:15 usiku.

  Baada ya mchezo huo, Sakho akateuliwa Mchezaji Bora wa Mechi za kuzawadiwa kitita cha Sh. 500,000.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI SIMBA NA AZAM FAINALI MAPINDUZI ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top