• HABARI MPYA

  Friday, January 28, 2022

  REFA KOMBA APEWA MAJUKUMU MENGINE NA CAF


  SHIRIKISHO la Soka Afrika limemteua refa wa Tanzania, Frank Komba katika orodha ya Waamuzi watakaochezesha mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Raja Club Athletic na Amazulu ya Afrika Kusini.
  Mechi hiyo itafanyika Februari 12, mwaka huu Uwanja Wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco na Kombe atakwenda huko baada ya kumaliza majukumu yake ya sasa kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Cameroon kwa sasa.


  Aidha, CAF pia imemteua Meneja Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto kuwa Mratibu wa mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa baina ya wenyeji, Mamelodi Sundowns na Al Hilal ya Sudan Februari 11 nchini Afrika Kusini.


  Naye Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo ameteuliwa na CAF kuwa Ofisa Habari wa mchezo wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho kati ya wenyeji, Simba SC na ASEC Mimosas ya Ivory Cost utakaochezwa Februari 13 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA KOMBA APEWA MAJUKUMU MENGINE NA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top