• HABARI MPYA

    Sunday, June 21, 2026

    JAPAN YAIPIGA TUNISIA 4-0 NA KUIONYESHA MLANGO WA KUTOKEA KOMBE LA DUNIA


    TIMU ya Japan imeibabua Tunisia mabao 4-0 katika mchezo wa Kundi F Fainali za Kombe la Dunia Asubuhi ya leo Uwanja wa BBVA, Guadalupe, Nuevo León nchini Mexico.
    Mabao ya Japan yamefungwa na kiungo wa Crystal Palace ya England, Daichi Kamada dakika ya nne na washambuliaji Ayase Ueda wa Feyenoord ya Uholanzi dakika ya 31 na 83 na Junya Itō wa KRC Genk ya Ubelgiji dakika ya 69.
    Ikumbukwe mchezo uliotangulia wa Kundi F jana usiku Uholanzi iliitandika Sweden mabao 5-1 Uwanja wa NRG, Houston, Texas, Marekani.
    Mabao ya Uholanzi ‘Orange’ yalifungwa na washambuliaji wanaocheza England watupu, Brian Ebenezer Adjei Brobbey wa Sunderland, mawili dakika ya tano na 17, Cody Mathès Gakpo wa Liverpool dakika ya 47 na 54, wote wana asili ya Ghana – huku lingine likifungwa na winga wa West Ham United, Crysencio Jilbert Sylverio Cirro Summerville mwenye asili ya Suriname dakika ya 89.
    Bao pekee la Sweden ambayo mechi ya kwanza nayo ilishinda 5-1 dhidi ya Tunisia – lilifungwa na mshambuliaji wa Newcastle United ya England pia, Anthony David Junior dakika ya 59.
    Msimamo wa Kundi F sasa baada ya mechi mbili za mwanzo, Uholanzi kileleni kwa pointi zake nne ikiizidi tu wastani wa mabao Japan, Sweden nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu – wakati Tunisia iliyopoteza mechi zote mbili za mwanzo inashika mkia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JAPAN YAIPIGA TUNISIA 4-0 NA KUIONYESHA MLANGO WA KUTOKEA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top