• HABARI MPYA

  Monday, January 31, 2022

  BEKI MZANZIBARI, SEBBO AONGEZA MIAKA MIWILI AZAM FC


  BEKI Mzanzibari, Abdallah Kheri 'Sebbo' ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuchezea Azam FC.
  Sebbo amesaini mkataba huo leo mbele ya Mtendaji Mkuu wa klabu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na sasa ataendelea kupiga kazi timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Bakhresa na familia yake hadi mwaka 2024.
  Aidha, Azam pia imeingia mkataba wa miaka mitatu na Omar Abdikarim Nasser, kuwa Kocha Msaidizi mpya, chini ya Msomali mwenzake, Abdihamid Moallin.


  Nasser amewahi kufanya kazi katika nchi mbalimbali, mara ya mwisho 2019, akiitumikia moja ya vigogo vya nchini Qatar, Al Sadd, akiwa kama mchambuzi wa mechi (analyst) wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 (U-23), kabla ya kufanya majukumu kama hayo akiwa Al Duhail ya huko pia.
  Al Sadd ni moja ya timu kubwa nchini humo, iliyokuwa ikinolewa na gwiji wa zamani wa Hispania, Xavi Hernandez, kabla kurejea Barcelona, akiwa kama Kocha Mkuu.
  Omary, mzaliwa wa Somalia aliyekulia England na kuchukua uraia wa huko, pia alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Somalia kuanzia mwaka jana hadi sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  Vinay said... February 8, 2022 at 1:17 PM

  Thank you for sharing useful information with us. please keep sharing like this. And if you are searching a unique and Top University in India, Colleges discovery platform, which connects students or working professionals with Universities/colleges, at the same time offering information about colleges, courses, entrance exam details, admission notifications, scholarships, and all related topics. Please visit below links:


  Mahakaushal University in Jabalpur

  YBN University in Ranchi

  Manipal University Jaipur

  Swami Vivekanand University in Sagar


  Item Reviewed: BEKI MZANZIBARI, SEBBO AONGEZA MIAKA MIWILI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top