• HABARI MPYA

  Monday, January 17, 2022

  SIMBA NA DAR CITY, YANGA NA MBAO FC 32 BORA ASFC


  MABINGWA watetezi, Simba SC watamenyana na Dar City katika Hatua 32 Bora na 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Katika droo iliyofanyika leo studio za AzamTv, Tabata Jijini Dar es Salaam, washindi wa pili wa msimu uliopita, Yanga SC watamenyana na Mbao FC, wakati Azam FC watacheza na Transit Camp na vigogo wote hao watatu watakuwa nyumbani.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA DAR CITY, YANGA NA MBAO FC 32 BORA ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top