• HABARI MPYA

  Thursday, January 27, 2022

  MISRI YATINGA ROBO FAINALI AFCON, IVORY COAST NA MALI NJE


  MABINGWA wa kihistoria, Misri wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa  penalti 5-4 dhidi ya Ivory Coast kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 Uwanja wa Douala nchini Cameroon.
  Waliofunga penalti za Misri ni Ahmed Mostafa Mohamed Sayed ‘Zizo’, Amr El Soleya, Omar Kamal, Mohamed Abdelmonem na Mohamed Salah.
  Upande wa Ivory Coast waliofunga ni Nicolas Pépé, Ibrahim Sangaré, Gnaly Cornet na Wilfried Zaha, wakati mkwaju wa Eric Bailly ulipanguliwa na kipa Mohamed Abou Gabal aliyeingia dakika ya 88 kufuatia Mohamed El Shenawy kuumia.
  Mechi ya mwisho ya Hatua ya 16 Bora, Equatorial Guinea pia ilitinga Robo Fainali kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 6-5 baada ya sare ya bila kufungana na Mali Uwanja wa Limbe.
  Robo Fainali zitaanza Jumamosi, wenyeji Cameroon wakimenyana na Gambia, Burkina Faso na Tunisia, Jumapili Misri na Morocco Na Senegal dhidi ya Equatorial Guinea, wakati Nusu Fainali zitafuatia Februari 2 na 3 na Fainali ni Februari 6.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MISRI YATINGA ROBO FAINALI AFCON, IVORY COAST NA MALI NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top