• HABARI MPYA

  Thursday, January 13, 2022

  REAL WAIPIGA BARCA 3-2, WATINGA FAINALI SUPER CUP


  TIMU ya Real Madrid imefanikiwa kutinga Fainali ya Super Cup ya Hispania baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Barcelona katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 usiku wa Jumatano Uwanja wa King Fahd International Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
  Mabao ya Real Madrid yamefungwa na Vinicius Junior dakika ya 25, Karim Benzema dakika ya 72 na Federico Valverde dakika ya 98, wakati ya Barcelona yamefungwa na Luuk de Jong dakika ya 41 Ansu Fati dakika ya 83.
  Real sasa itakutana na mshindi kati ya Atletico Madrid na Athletic Club zinazomenyana leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL WAIPIGA BARCA 3-2, WATINGA FAINALI SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top