• HABARI MPYA

  Tuesday, January 18, 2022

  CAMEROON YAMALIZA MAKUNDI BILA KUPOTEZA MECHI


  WENYEJI, Cameroon wamekamilisha mechi zao za Kundi A bila kupoteza hata moja baada ya kutoa sare ya 1-1 na Cape Verde usiku wa Jumatatu Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaoundé.
  Vincent Aboubakar alianza kuwafungia Cameroon dakika ya 39, kabla ya Garry Rodrigues kuisawazishia Cape Verde dakika ya 53.
  Mechi nyingine ya Kundi hilo, Burkina Faso pia ilitoa sare ya 1-1 na Ethiopia Uwanja wa Bafoussam .
  Cameroon inamaliza na pointi saba, ikifuatiwa na Burkina Faso pointi nne ambayo pia inafuzu Hatua ya mtoano kwa kuizidi wastani wa mabao Cape Verde, wakati Ethiopia imeshika mkia na pointi yake moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YAMALIZA MAKUNDI BILA KUPOTEZA MECHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top