• HABARI MPYA

  Friday, January 21, 2022

  MBEYA KWANZA YAAMBULIA SARE KWA KMC 1-1 SOKOINE


  WENYEJI, Mbeya Kwanza wamelazimishwa sare ya 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Matheo Anthony alianza kuifungia KMC dakika ya pili tu, kabla ya mshambuliaji mwenzake, Habib Kyombo kuisawazishia Mbeya Kwanza dakika ya 90 na ushei.
  Kwa sare hiyo, Mbeya Kwanza wanafikisha pointi 12 katika mchezo wa 13 ingawa wanabaki nafasi ya 11 na KMC wanatimiza pointi 15 katika mchezo wa 13 pia na kusogea nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA KWANZA YAAMBULIA SARE KWA KMC 1-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top