• HABARI MPYA

  Thursday, January 13, 2022

  RUVU SHOOTING YASAJILI SABA WAPYA KUIMARISHA KIKOSI LIGI KUU


  KLABU ya Ruvu Shooting ya Pwani imeimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji saba wapya kuelekea sehemu iliyobaki ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Hao ni kipa Benedict Tinocco, beki Iddi Mfaume Mobby kutoka Geita Gold, winga Haroun Chanongo na mshambuliaji Abalkassim Suleiman kutoka Mtibwa Sugar.
  Wengine ni kiungo Hussein Suleiman ‘Chuse’ kutoka Mbao FC ya Mwanza, beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Jaffar Mohamed kutoka Namungo FC na mshambuliaji Hamad Rajab Majimengi kutoka Coastal Union ya Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YASAJILI SABA WAPYA KUIMARISHA KIKOSI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top