• HABARI MPYA

  Sunday, January 09, 2022

  YANGA YAPONGEZA WANA YANGA KUTEULIWA NA RAIS


  UONGOZI wa Yanga umewapongeza wapenzi na wanachama wake walioteuliwa na Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kuongoza Wizara na Idara mbalimbali za Serikali katika uteuzi uliofanywa jana.
  Miongoni mwa Yanga walionufaika na uteuzi huo uliofanywa jana ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete ambaye anakuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini ya Waziri Dk. Angelina Mabula. 
  Mwingine ni Kapteni George Huruma Mkuchika anayeendelea kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) ambayo awali ilikuwa Wizara ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAPONGEZA WANA YANGA KUTEULIWA NA RAIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top