• HABARI MPYA

  Sunday, January 30, 2022

  SIMBA SC YAFUTA GUNDU KWA DAR CITY, YAICHAPA 6-0


  MABINGWA watetezi, Simba SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Dar City usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na wageni watupu, mshambuliaji Mnyarwanda mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere mawili dakika ya tano na 13, viungo Wazambia, Clatous Chama dakika ya 18 na Rally Bwalya dakika ya 22, beki Muivory Coast, Pascal Wawa dakika ya 48 na mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu dakika ya 80.
  Mechi nyingine za 32 Bora leo, Mtibwa Sugar imewatoa wenyeji, African Sports kwa penalti 4-2 baada y sare ya 0-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na Kagera Sugar imewachapa wenyeji, African Lyon 4-0, Meshack Abraham akipiga hat trick, lingine akifunga Abeid Athumani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAFUTA GUNDU KWA DAR CITY, YAICHAPA 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top