• HABARI MPYA

    Thursday, January 13, 2022

    SIMBA SC MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI 2022


    BAO la penalti la mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddi Kagere limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Kagere alifunga bao hilo dakika ya 56 baada ya winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho kugongana na kipa Mganda wa Azam FC, Mathias Kigonya na hilo linakuwa taji la nne la Mapinduzi kwa Simba baada ya awali kulibeba mwaka 2008, 2011 na 2015.
    Baada ya mchezo, beki Mkongo, Hennock Inonga Baka ‘Varane’ alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi, wakati winga Sakho alichaguliwa Mchezaji Bora wa Mashindano, Aishi Manula Kipa Bora na Kagere Mfungaji Bora huku chipukizi Tepsi Evance wa Azam FC alipewa Tuzo ya Mchezo wa Kiungwana.
    Aishi, Baka, Kagere na Sakho kila mmoja alipewa Sh. Milioni 2, wakati Tepsi alipewa Sh. 300,000.


    Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi alimkabidhi Nahodha wa Simba Kombe na mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 25, wakati Azam FC walipewa Sh. Milioni 15.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top