• HABARI MPYA

  Thursday, January 13, 2022

  CAMEROON YAICHAPA ETHIOPIA 4-1, YASONGA MBELE AFCON


  WENYEJI, Cameroon wamekuwa timu ya kwanza kuingia hatua ya mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Ethiopia  katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Paul Biya Jijini Yaoundé.
  Mabao ya Cameroon yamefungwa na Karl Toko Ekambi mawili dakika ya nane na 67 na Vincent Aboubakar mawili pia dakika ya 53 na 55, baada ya Wahabeshi kutangulia kwa bao la Dawa Hottesa dakika ya nne.


  Mechi nyingine ya Kundi A leo, Burkina Faso imeilaza Cape Verde 1-0, bao pekee la Boureima Hassane Bandé dakika ya 39 hapo hapo Paul Biya.
  Kwa matokeo hayo, Simba Wasiofungika wanafikisha pointi sita baada ya mechi ya mbili na kuendelea kuongoza Kundi A wakifuatiwa na Burkina Faso na Cape Verde wenye pointi tatu kila moja, wakati Ethiopia inaendelea kushika mkia ikiwa haina pointi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YAICHAPA ETHIOPIA 4-1, YASONGA MBELE AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top