• HABARI MPYA

  Friday, January 21, 2022

  JOTA AIPELEKA LIVERPOOL FAINALI CARABAO CUP


  MABAO ya Diogo Jota dakika ya 19 na 77 yameipa Liverpool ushindi wa 2-0 wa dhidi ya wenyeji, Arsenal katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Jota alifunga mabao hayo Nara zote akimalizia kazi nzuri za Trent Alexander-Arnold na kufuatia sare ya 0-0 kwenye mechi ya kwanza Anfield wiki iliyopita, wanakwenda fainali ya Carabao Cup na watakutana na Chelsea Februari 27 Uwanja wa  Wembley Jijini London. 
  Kwa mara nyingine kocha Jurgen Klopp alikuwa mwenye bahati baada ya wapinzani kumaliza pungufu kufuatia Thomas Partey kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90, yaani dakika 16 tangu aingie kuchukua nafasi ya Emile Smith Rowe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOTA AIPELEKA LIVERPOOL FAINALI CARABAO CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top