• HABARI MPYA

  Monday, January 24, 2022

  LIVERPOOL YAITANDIKA CRYSTAL PALACE 3-1 SELHURST PARK


  TIMU ya Liverpool imewachapa wenyeji, Crystal Palace mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumapili Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Virgil van Dijk dakika ya 18, Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 32 na Fabinho kwa penalti dakika ya 89, wakati la Crystal Palace limefungwa na Odsonne Edouard  dakika ya 55.
  Liverpool inafikisha pointi 48 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tisa na Manchester City ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake 24 za mechi 22 katika nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAITANDIKA CRYSTAL PALACE 3-1 SELHURST PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top