• HABARI MPYA

  Monday, January 17, 2022

  WENGINE WASHINDA MAMILIONI SPORTPESA JACKPOT BONUS


  WAKAZI wa Geita, Iringa, Dar es Salaam, Zanzibar na Tunduma mkoani Songwe wameibuka washindi wa Jackpot Bonus ya Sportpesa kwa kushinda  timu 12, 11 na 10 mwisho
  ni mwa wiki iliyopita.
  Wakizungumza baada ya utambulisho na makabidhiano ya mfano wa hundi washindi hao wakiongozwa na Bw. Enos Nzagamba, ambaye ameshinda mechi 12 mfululizo, kwa mara ya tatu, ndani ya miezi minne, amesema ana imani ipo siku atashinda Jackpot hiyo  ambayo kwa sasa imesimamia Tshs 846,297,200 kwa wiki hii.
  “Mimi najitahidi sana kufukuzia hii Jackpot kwa bahati mbaya mechi niliyoikosa ya Villareal dhidi ya Ateltico Madrid haikwenda nilivyoipigia hesabu.
  Naye David Kilunga pamoja na Mohamed Hamadi, Emmanuel Mhagama, Willium Sichula na Adolf Chandi kwa nyakati tofauti wamesema wataendelea kucheza Jackpot ya Sportpesa kwa kuwa odds zao pamoja na malipo yanawapa uthubutu wa kujiamini kuifukuzia Jackpot hiyo kila mwisho wa wiki.
  “Mimi nacheza kwa urahisi kabisa kwa kutumia simu yangu ya kitochi mpaka sasa. Nilianza kucheza mwaka 2017 na sijawahi kuacha.” Alisema Emmanuel Mhagama.
  Akiunga mkono hoja ya Bw. Emmanuel, Bw. Adolf amesema yeye kuwa anatumia njia ya Quick pick ama kwa lugha rahisi ni uchaguzi wa haraka amewahi kushinda mara kadhaa.
  ‘’Ninaipenda sana njia ya Quick Pick kwani njia hii inakuchagulia yenyewe na pia kama hujaridhishwa na machaguo yake unaweza kuchanganua mwenyewe na kurekebisha kwa namna unayotaka.
  Washindi wote kwa Pamoja wamewaasa watanzania kucheza na Sportpesa kwa kuwa ndiyo njia ya uhakika na salama kushinda fedha za ubashiri kwa kutumia Jackpot.
  Kila wiki kama Jackpot haikupata mshindi basi dau huongezeka na tangu kupatikana mshindi mnamo mwaka jana Jackpot ilishuka hadi Tsh 200,000,000 na kuendelea kuongezeka kila wiki hadi sasa kufikia Tshs846,297,200.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGINE WASHINDA MAMILIONI SPORTPESA JACKPOT BONUS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top