• HABARI MPYA

    Tuesday, January 25, 2022

    SITA WAFARIKI WAKIGOMBEA KUINGIA UWANJANI CAMEROON


    WATU wasiopungua sita wamefariki na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea nje ya Uwanja wa Olembe Jijini Yaounde wakigombea kuingia kutazama mechi baina ya wenyeji wa Fainali za AFCON, Cameroon dhidi ya Comoro jana – Serikali ya nchi hiyo imethibitisha na kusema kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka.
    Maafisa wa hospitali ya Messassi wamesema wamepokea kiasi cha watu 40 waliojeruhiwa, ambao walikimbizwa hospitalini hapo na Polisi na wasamaria wema – na chanzo cha vurugu hizo imeelezwa ni walinzi ‘Stewards’ kufunga mageti kuzuia watu zaidi kuingia uwanjani – na baada ya tafrani hiyo ilishuhudiwa viatu, kofia na mawigi vikizagaa chini.
    Katika mechi hiyo ya Hatua ya 16 Bora, Cameroon ilishinda 2-1 na kwenda Robo Fainali.
     Pamoja na hayo, Hatua ya 16 Bora ya AFCON inaendelea leo kwa mechi mbili, washindi wa pili wa 2019 Senegal wakimenyana na Cape Verde Saa 1:00 usiku na Morocco dhidi ya Malawi Saa 4:00 usiku.
    Kocha wa Morocco, Vahid Halilhodzic amesema kambi yake imetikiswa mno na janga la COVID kuelekea mchezo wake na Malawi, japokuwa beki Achraf Hakimi alifanya mazoezi jana baada ya siku nzima ya Jumapili kupumzika tu hotelini.
    Lakini bado haijulikani kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 atakuwa sehemu ya mchezo wa leo Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaounde.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SITA WAFARIKI WAKIGOMBEA KUINGIA UWANJANI CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top