• HABARI MPYA

  Saturday, January 29, 2022

  JULIANA RUGUMISHA KUIWAKILISHA TANZANIA FACE AFRICA


  BINTI Juliana Rugumisha, amepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Future Faces Africa Grand Finale 2022 yanayotarajia kufanyika jumapili januari 30 2022, nchini Nigeria.
  Juliana ambaye ni miss Tanzania 2021 amepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Future faces Africa 2022 nchini Nigeria ambapo washindi 12 watakaopatikana wataingia kandarasi ya miaka miwili na kampuni ya FFA katika masuala ya mitindo.
  Future Face imejikita katika kutafuta wanamitindo ndani ya Afrika na kushiriki katika shindano hilo la kipekee na mfano na ni moja ya mashindano makubwa kuwahi kutokea.
  Mwanzilishi wa FFA na mmiliki wa moja ya wakala mkubwa wa Modeling barani Afrika, Elizabeth Elohor, amesema Katika miaka iliyopita Dunia imeshuhudia ongezeko kubwa la kutambuliwa na kuthaminiwa kwa wanamitindo wa kiafrika na mitindo ya kiafrika ikipatiwa nafasi kubwa ulimwenguni.
  Alisema, washindani 12 wanaoshindania nafasi ya kushinda kandarasi ya uana mitindo ya kimataifa ya miaka 2 na wakala wa juu wa uanamitindo wa kimataifa.                                                                                                      Washindi  watazawadiwa pesa taslimu $5,000 sawa na Milioni 11 za kitanzania kwa washindi wa kiume na wa kike.


  Elizabeth alisema, shindano hili sio tu kuwapa wahitimu waliofaulu taaluma ya uanamitindo tu, bali pia  kazi katika jukwaa la dunia.
  Akizungumza kuelekea shindano hilo siku ya kesho nchini Nigeria,Elizabeth alisema walitamani kufika Tanzania ila Mlipuko wa ugonjwa wa Covie -19 umekuwa ni changamoto.  Wanaamini mwaka 2024 watafika kutafuta vipaji vipya.
  Ameongeza kuwa, wamefurahi uwepo wa mwakilishi kutoka Tanzania Juliana Rugumisha, kuiwakilisha Taifa lake na wanamtakia kila la heri kwenye shindano la Future Faces Africa Grand Finale 2022.     
   
  Akiongea kwa njia ya simu,  Millen Magese, ambaye ni MWANAMITINDO wa kimataifa nchini New york na pia Mkurugenzi wa MMG(Kampuni iliyojikita zaidi kwa kuitangaza Tanzania, Kimataifa kupitia  uanamitindo  na mitindo kutoka Tanzania na kpatia fursa ndani ya Afrika na dunia nzima.
  "Hii ni nafasi nyingine na kubwa zaidi kwa vijana wetu wa kike na kiume , Mwaka huu ameenda mshiriki mmoja mwakani vijana wajipange kwa ajili ya kushiriki na wadhamini , wajitokeze kwa ajili ya kuunga mkono mashindano hayo.
  Kwa upande wa mshiriki Juliana ambae yupo Lagos Nigeria alisema amejiandaa vizuri kuhakikisha anaiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ambayo ni makubwa Afrika na kuwa kati ya moja ya washindi.
  Juliana alisema, uwepo wake katika mashindano hayo ni chachu kwa mabinti wengine wanaopenda masuala ya urembo na ulimbwende nchini.
  Kati ya zao la FFA ni Super model  Mayowa Nicolas,(Nigeria) Davinson (Nigeria), Nyangua ( Zimbawe) na wengine wengi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JULIANA RUGUMISHA KUIWAKILISHA TANZANIA FACE AFRICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top