• HABARI MPYA

  Friday, September 08, 2017

  MECHI YA AZAM NA SIMBA YARUDISHWA SAA 10:00 JIONI KWA SABABU ZA KIUSALAMA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Azam FC na Simba SC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, umerudishwa Saa 10:00 jioni kutoka Saa 1:00 usiku.
  Hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama, baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kusema kwamba ni hatari mechi hiyo kuchezwa usiku na imeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuirudisha Saa 10:00 jioni.
  Mambo mengine yote yanabaki kama yalivyopangwa na mchezo huo utachezeshwa na refa Ludovick Charles wa Tabora, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Abdallah Mkomwa wa Pwani na mezani atakuwepo Josephat Bulali na Kamisaa  atakuwa Ruvu Kiwanga, wote wa Dar es Salaam, wakati viingilio ni Sh. 10,000 kwa jukwaa la VIP na 7,000 kwa mzunguko.
  Mashabiki wa Simba wanatarajiwa kumiminika kwa wingi Chamazi kesho
  Timu zote zilianza kwa ushindi katika mechi zao za kwanza Ligi Kuu, Azam FC wakishinda 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara huku Simba wakishinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Na kesho makocha wa timu zote, Mcameroon Joseph Marius Omog na Mromania Aristica Cioaba watataka kuendeleza wimbi la ushindi katika jitihada za kuipokonya taji Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI YA AZAM NA SIMBA YARUDISHWA SAA 10:00 JIONI KWA SABABU ZA KIUSALAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top