• HABARI MPYA

  Sunday, April 09, 2023

  TANZANIA PRISONS YAICHAPA RUVU SHOOTING 3-1 SOKOINE


  WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Jumanne Elfadhil dakika ya sita na Jeremiah Juma, mawili dakika ya 41 na 50, baada ya Valentino Mashaka kuanza kuifungia  Ruvu Shooting dakika ya pili.
  Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya 10, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 20 nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi 26.
  Ikumbukwe mwishoni mwa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja, wakati watakaomaliza nafasi ya 13 na 14 watamenyana baina yao timu itakayofungwa baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini itakwenda kucheza timu ya Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAICHAPA RUVU SHOOTING 3-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top